TUME HURU YA UCHAGUZI HAIWEZI KUCHUKUA MAAGIZO KUTOKA KWA MTU MWINGINE

 

Tume huru ya uchaguzi nchini kenya amesema tume hiyo ni huru na  haiwezi kuchukua maagizo kutoka kwa mtu mwingine kuhusu maandalizi mapya ya uchaguzi oktoba 17 mwaka ujao.

Mwenyekiti wa tume hivyo wafula chebukati ametoa kauli hiyo  baada ya chama cha jubilee cha rais uhuru kenyatta na muungano wa upinzani nasa, kuiandikia barua tume hiyo kupinga watendaji wapya waliotangazwa hivi karibuni iliyoeleza kuwa mabadiliko hayo yanafanyika kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo .

Nasa, inataka baadhi ya wafanyikazi wa tume hiyo kuachishwa kazi akiwemo mkurugenzi mkuu ezra chiloba wakati chama cha jubilee pia kimepinga  mabadiliko yaliyofanyika kwa madai kuwa  watendaji hao wapya wanaegemea mrengo wa kisiasa