TUME YA HAKI ZA BINADAMU IMEIPONGEZA S KWA KUTOA PESHENI KWA WAZEE.

Tume ya haki za binadamu na utawala bora imeipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutoa pesheni kwa wazee.

Pongezi hiyo imetolewa na mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora Bahame Tom Iyanduga katika siku ya kupinga mateso na ukatili dhidi ya wazee dunia

Aidha nyanduga amesema licha ya kuwepo kwa sera ya wazee lakini bunge bado halijatunga sheria inayoianisha  kulinda haki za wazee.

Kwa upande wa mwakilishi wa taasisi ya wazee wastaafu zanzibar(viwaza) Dkt. Yusufu Nuh Pandu ameiomba serikali ya mapinduzi Zanzibar kuongeza posho ya pesheni kwa wazee pamoja na kushusha  umri wa wanufaika wa  pesheni kutoka miaka 70 hadi 60.

Kwa mujibu wa sera ya watu na makazi ya mwaka 2002 inaonyesha asilimia 5.6 ya watanzania ni wazee ambapo asilimia 80 ya wazee hao wanaishi vijijini na  asilimia 50wanaishi na  watoto yatima.

Kauli mbiu ya siku ya siku ya kupinga mateso na ukatili dhidi ya wazee duniani ni elewa na kukomesha unyanyasaji wa kipato kwa wazee –haki za binadamu