TUME YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA IMEJIPANGA KUFANYA UHAKIKI WA VIONGOZI

 

Tume  ya  maadili  ya  viongozi  wa  umma  imesema  imejipanga  kufanya   uhakiki  wa viongozi  wa  umma  ili kufuatilia mali  na  madeni  ya  viongozi  hao  na kujua taarifa  zao

Akitoa  mafunzo  kwa  masheha  na  madiwani  wa  wilaya  ya  magharib  ‘a’  juu  ya  kutambua  maadili  ya  viongozi  wa  umma,na  afisa  muandamizi  wa  tume ya  maadili  ya viongozi  wa  umma  said  abdalla  natepe amesemauhakikim huo utasaidia  serikali  kujua  jinsi  gani viongozi  wake  wanavyotekeleza  kazi zao  na mali  walizonazo  walivyozipata.

Kwa upande wao washiriki  wa  mafunzo  hayo  wamesema  mafunzo  hayo  yatawajengea  uwezo mzuri  wa  kujiamini  wanachokifanya  pamoja  na  kuwa   waadilifu.

Mapema  akifungua  mafunzo  hayo  mkuu  wa  wilaya  ya magharib  a  kapten  khatib  khamis  amewataka  masheha  na  madiwani  kuwa  makini  kwani  mafunzo   hayo  yatawapa  uelewa  juu  ya  kujua   wajibu   wao   katika  kazi  na  kuweza  kutekeleza  vyema  kwa  mujibu  wa  sheria.

Mafunzo  hayo  ya  siku  moja  yatatoa  fursa  kwa  viongozi  wa  umma  kuwa   waadilifu   kwa   kuzitambua  na  kuzikagua   mali  wanazomiliki.