TUME YA UTUMISHI IMETAKIWA KUFANYA KAZI ZAKE KWA UWADILIFU ILI KUEPUKA MALALAMIKO

Tume ya utumishi serikalini imetakiwa kufanya kazi zake kwa uwadilifu ili kuepuka malalamiko yanayotolewa na wananchi juu ya utowaji wa ajira kwa njia ya upendeleo.
akizindua bodi mpya ya tume ya utumishi serikalini waziri wa nchi ofisi ya rais katiba sheria utumishi wa umma na utawala bora mhe haroun ali suleiman ameitaka tume hiyo kufanya kazi kwa haki, uwazi, na uwadilifu ili kuepuka malalamiko yanayojitokeza mara mara wakati wa uwajiri.
Amesisitiza suala la uwajibikaji katika taasisii za serikali kwani kumekuwa na wimbi kubwa la wafanyakazi katika taasisi mbali mbali hawafanyi kazi zao kwa mujibu wa sheria za utumishi .
Naibu katibu mkuu ofisi ya rais katika sheria utumishi wa umma na utawala bora seif shaaban mwinyi ameita tume hito kufanya kazi zake kwa mashirikiano na serikali ili kupunguza wimbi la mamaliko wakati wa ajira .
Katibu tume ya utumishi serikalini mohamed khamis mohamed amesema kumejitokeza kwa baadhi ya wakuu wa taasisi za serikali kuchelewa kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wanaokwenda kinyume na taratibu za utumishi hali ambayo huiweka tume katika wakati mgumu hasa inapotaka kufanya maamuzi.
Akitoa shukurani mwenyekiti mpya wa tume ya utumishi serrikalini othmana bakari othman amesema tumeyake itajitahidi kusiamia kwa makini ajira zinazotolewa kwa wananchi ili kuweza kuondokana na malalamiko yanayojitokeza.
Katika hafla hiyo kumetolewa vyeti vya shukrani kwa bodi iliyomaliza muda wake wa uwongozi katika kipindi cha miaka mitatu.