TUTAENDELEZA UTAMADUNI WA KUBADILISHANA UZOEFU KWA PANDE MBILI ZA MUUNGANO

Mkuu wa mkoa mjini magharib Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amesema serikali ya mkoa wa mjini magharibi itaendeleza utamaduni wa kubadilishana uzoefu kwa pande mbili za muungano katika maeneo mbalimbali ya uwekezaji ili kuona lengo la serikali la kuleta maendeleo wananchi wake linafikiwa.

Akizungumza katika muendelezo wa ziara kwa mkoa wa rukwa Mhe Ayoub amesema pamoja na kutekeleza maagizo na maelekezo ya serikali, uongozi wa mkoa wa mjini mgharibi utendelea kushirikiana kwa karibu na mikoa mbalimbali katika kujifunza na kuongeza thamani ya bidhaa zinazopatikana ndani ya nchi.

Aidha Mh: Ayoub ameridhishwa na uwezo wa chinjio la saafi katika maeneo ya uchinjaji na uzalishaji bidhaa zipatikanazo kiwandani hapo na kuahidi kushauri vizuri serikali katika uimarishaji wa machinjio mbalimbali nchini.

Akitoa maelezo ya chinjio hilo afisa mfawidhi wa kituo cha uchunguzi wa maradhi ya wanyama na daktari mkuu wa kiwanda cha nyama cha  saafi Dr Kaini Martin Kamwela amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuchinja ng’ombe miatatu kwa siku pamoja na ziada ya wanyama wadogo wadogo kama mbuzi na kondoo.

Akizunguza mara baada ya kupokea ujumbe huo mkuu wa wilaya ya sumbawanga Dr Khalfany Haule ameuomba uongozi wa serikali ya mkoa wa mjini kutumia uwezo na nafasi walionayo kuwatafutia wawekezaji kiwanda cha saafi katika mifugo na maziwa kutokana wingi wa ng’ombe walipo wilayani hapo.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App