TUZO 15 KWA WACHEZAJI, TIMU NA WAAMUZI WALIOFANYA VIZURI

Usiku wa Mei 24, 2017 tuzo za tanzani bara zilitolewa KWA WACHEZAJI, TIMU NA WAAMUZI WALIOFANYA VIZURI katika kipindi chote cha msimu wa 2016/2017 ambapo zilitolewa TUZO TAKRIBANI 15 kwenda kwa watu mbalimbali.
Katika hafla hiyo, tuzo kubwa ambayo ilikua ikisubiriwa kwa hamu ilikuwa ni ya mchezaji bora wa msimu ambao ulimalizika Mei 20 na Yanga kuibuka mabingwa baada ya kuchukua taji la ligi hiyo ikiwa ni kwa mara ya tatu mfululizo huku ikiwa ni mara ya 27 kihistoria.
Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora ilinyakuliwa na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ beki wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Tshabalala amewashinda golikipa wa Azam Aishi Manula, Simon Msuva kutoka Yanga, kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima na Shiza Kichuya wa Simba.
Beki huyo wa kushoto alifanikiwa kucheza mechi zote za ligi kwa dakika 90 za kila mchezo huku akipata kadi mbili tu za njano na kuisaidia timu yake kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Tuzo hiyo ilipokelewa na baba mzazi wa mchezji huyo Mzee Hussein Zimbwe kutokana na mchezaji mwenyewe kutokuwepo kwenye hafla ya utoaji wa tuzo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ndiyo alikabidhi tuzo hiyo.