UAE YASHUTUMIWA KUIDUKUA QATAR

Mzozo wa ghuba ya kiarabu umechukua sura mpya, baada ya ripoti kudai umoja wa falme za kiarabu (uae) umechunguza tovuti ya qatar, na kuingiza ripoti ilitumiwa kuiwekea vikwazo nchi hiyo.
Ripoti hiyo imedai sheikh al-thani amesema iran ni nchi muhimu yenye nguvu katika kanda, haiwezi kupuuzwa, na si jambo la busara kugombana nayo.
Wiki iliyopita waziri wa mambo ya nje wa marekani rex tillerson alizuru katika ghuba ya kiarabu kujaribu kutafuta suluhu ya mzozo huo bila mafanikio kwa muda wa siku nne.