UAMINIFU NA UWAJIBIKAJI KWA WAFANYAKAZI WA OFISI YA NYARAKA NDIO KITU MUHIMU

 

 

Naibu waziri wa habari utalii na mambo yake mh, chumu kombo khamis amesema uaminifu na uwajibikaji kwa wafanyakazi wa ofisi ya nyaraka ndio kitu muhimu katika sehemu yao ya kazi ili kuleta ufanisi wa taasisi hiyo.

Amesema idara ya nyaraka  ndio sehemu muhimu ya kuhifadhi na kuhakiki kumbu kumbu mbali mbali ili ziweze kutumika kwa matumizi ya baadae ikiwa ni pamoja na kusaidia kufanya tafiti mbali mbali.

Mh, chumu ameyasema hayo huko ukumbi wa nyaraka na mambo ya kale wakati akizungumza na wafanyakazi wa ofisi hiyo.

Akizungumzia suala la utunzaji wa maeneo ya kihistoria amesema eneo la mkama ndume lina kila sababu ya kurudishwa katika uhalisia wake hivyo ni vyema kuwashirikisha wananchi katika suala la utunzaji wa eneo hilo.

Naye afisa mdhamini wa wizara ya habari utalii na mambo ya kale pemba khatib juma mjaja amemuhakikishia naibu waziri huyo kwamba ofisi yake itatoa kila aina ya msaada utakao hitajika ili lengo la uwepo wa ofisi ya nyaraka liweze kufikiwa ikiwa ni pamoja na kujenga mshikamano miongoni mwa wafanyakazi  wa taasisi hiyo.

Kwa upande wao wafanyakazi hao wameahidi kushirikiana na kufanya kazi kwa uaminififu na uadilifu ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kama ilivyokusudiwa.