UAMUZI WA RAIS DONALD TRUMP KUUTAMBUA MJI WA JERUSALEM

 

Uamuzi wa rais Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel umesababisha ukosoaji mkubwa kutoka viongozi wa umoja wa ulaya na waarabu huku kukiwa na hofu kwamba uamuzi huo unaweza kuzusha ghasia zaidi katika eneo hilo.

Rais wa mamlaka ya palestina mahmoud abbas amesema tangazo la trump  linabadilisha sera ya marekani ya miongo kadhaa linapaswa kulaumiwa.

Rais wa uturuki recep tayyip erdogan amesema rais trump analitumbukiza eneo la mashariki ya kati katika ghasia.

Wajumbe wanane wa baraza la usalama la umoja wa mataifa ikiwa ni pamoja na uingereza, ufaransa, misri, italia na sweden wameitisha mkutano wa dharura ambao utafanyika kesho, kuhusiana na hatua hiyo ya marekani.

Maandamano makubwa yanaendela kufanyika nchini palestina kupinga uamuzi huo wa trump ambapo chama cha hamas kimesema kitaendela na maandamano mpaka haki itendeke.