UCHAGUZI WA MARUDIO WA MBUNGE WA JIMBO LA KINONDONI KUFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI

 

Jeshi la polisi mkoa wa kipolisi wa kinondoni dar-es-salaam limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha kuwa uchaguzi wa marudio wa mbunge wa jimbo la kinondoni unaotarajiwa kufanyika siku ya jumamosi  ya tarehe 17/02/2018 unafanyika kwa amani.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi kinondoni asp muriro jumanne muriro amesema tayari vikosi vya askari wa kutuliza ghasia, askari kanzu, na magari ya maji ya kuwasha viko katika hali ya tahadhali kuhakikisha mchakato wote wa masuala ya uchaguzi unafanyika kwa misingi ya sheria, kanuni na taratibuza uchaguzi.

Kamanda muriro akawatoa hofu wananchi walio na sifa za kupiga kura na kusema wasiwe na hofu pale watakapoona makundi ya askari.                  Vilevile kamanda muriro akakanusha uvumi juu ya kile kinachodaiwa kuwa jeshi la polisi lilivamia ofisi za chadema na kuwakamata viongozi wake na kusema waliokamatwa ni watu waliovamia barabarani.

Aidha kamanda muriro amesema jeshi la polisi linaendelea na uchungu ili kubaini chanzo cha kifo cha mtu ambaye mwili wake ulikutwa katik ufukwe eneo la cocobeach osterbay akidaiwa kuwa  alitekwa.