UCHAGUZI WA WABUNGE UFARANSA WAFANYIKA JUMAPILI

raia wa ufaransa wamepiga kura kuchagua wabunge ambapo chama kinachoongozwa na rais emanuel macron uchaguzi kikitazamiwa kupata ushindi mkubwa.

bunge jipya linatarajia kushuhudia mageuzi ya kuwepo wabunge vijana zaidi,wawanawake  kufuatia ushindi wa macron katika uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni.

vyama vyengine vimetoa wito wa kuungwa mkono ili kuepusha mamlaka yote kwenda kwa chama pekee cha macron.

chama kinahitaji viti 289 ili kuongoza bunge la kitaifa lenye jumla ya wabunge 577 ambapo sasa chama cha lrem kinachoongozwa na macron kinatazamiwa kupata zaidi ya viti 400.