UCHUMI WA NCHI UTAZIDI KUIMARIKA KUPITIA SEKTA YA UTALII.

Wakala wa ulinzi wa serikali wamesema iwapo taasisi zinazojishughulisha na ulinzi zitapata mafunzo mazuri na kufanyakazi kwa kufataa sheria uchumi wa nchi utazidi kuimarika kupitia sekta ya utalii.

Mkurugengi wa wakala wa ulinzi luteni kanal jabir hamza  na mwanasheria wa taasisi hiyo wamesema wawekezaji na wageni watashindwa kuwekeza na kushusha uchumi wa taifa iwapo kutakuwa hakuna usalama wa uhakika katika sekta hiyo.

Wamesema  kuwepo kwa sheria ya wakala wa ulinzi kutasaidi kuwa na usalama na uhakika wa kuwekeza na kuinua sekta ya utalii ambao nitegemeo kubwa  la uchumi.

Mkurugenzi hamza amesema kuundwa taasisi hiyo kutaondosha malalamiko ya vitendo viovu kwa wageni wanaotembelea zanzibar na kuitangaza vyema nchi.

Nao viongozi wa taasisi za ulinzi za kiraia kuhusu usajili wa taasisi zao wamesema chombo hicho kitasaidia kuwepo kwa mamlaka ambayo itasaidia kupata haki zao.

Wamesema pamoja na kulipia kodi na kuwapatia vijana ajira bado kuna umuhimu wa kuwepo chombo hicho ambacho kinafahamika rasmi.

Awali mwenyekiti wa bodi ya wakala wa ulinzi kanal mstaafu makame mabrouk  amesema  shughuli za ulinzi zinahitaji uzalendo na ndio ambao unaleta maendeleo katika nchi.