UDUNI WA VYOMBO KUNAKOSABABISHA KUSHINDWA KUFIKA BAHARI KUU

 

Wavuvi  katika mkoa wa kaskazini  unguja  wamesema  licha ya kuwepo kwa  rasilimali  kubwa ya samaki katika ukanda huo wanashindwa  kuvuna rasilimali hiyo  kutokana na uduni wa vyombo wanavyotumia  kunakosababisha  kushindwa  kufika bahari kuu

Wakizungumzia  hali ya halisi ya upatikanaji wa samaki katika kipindi hiki  cha  mvua za masika wamesema wanatumia nguvu kubwa na kupata tija ndogo kwa kutohimili misukosuko ya baharini pamoja  na  kuendelea na uvuvi wa kizamani.

Kufuatia hali hiyo  wavuvi  hao wamesema  wana   fursa  kubwa   ya  kuweza  kufaidika  na  kazi  zao  iwapo  watawezeshwa  kupata  vyombo   vya    kisasa  ili  kufika    kuvua  katika   kina  kikubwa     cha   bahari.

zbc haikuishia  hapo ilifika kwa  wauza samaki na kutaja bei tofauti za samaki ikiwemo  mkule mmoja shiling elfu kumi na mbili  mtande  wa pugu elfu nne chaa fungu elfu tano  na tuguu elfu nne