UGONJWA USIOFAHAMIKA UMESABABISHA VIFO VYA KAA WENGI KATIKA PWANI YA KENDWA HUKO NUNGWI

Ugonjwa usiofahamika umesababisha vifo vya kaa wengi katika pwani ya kendwa huko nungwi na kuzua hofu kwa wananchi wa maeneo hayo.
Wakizungumza na zbc wananchi wa kendwa wamesema tukio hilo limejitokeza muda wa wiki moja sasa na kuuwa kaa wengi wadogo wadogo wanaoishi katika maji yenye kina kirefu
Maafisa kutoka idara ya maendeleo ya uvuvi zanzibar wamesema wanafanya uchunguzi wa tukio hilo ili kujua nini kilichosababisha kufariki kwa kaa hao
Aidha idara ya maendeleo ya uvuvi imetoa wito kwa wananchi wa kendwa kutowatumia kwa matumizi ya chakula kwani hawako salama kwa matumizi ya binadamu