UHALIFU HALI INAYORUDISHA NYUMA MAENDELEO YA ELIMU SKULI YA KIJITOUPELE

 

 

Walimu wa skuli ya  abdallah sheria  ya kwarara wamelalamikia tatizo la  wahalifu ambbao wanaingia katika madarasa hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya elimu katika skuli hiyo.

Mwalimu mkuu wa skuli  hiyo nd  haji juma ametoa kero  hiyo walipombelewa na mwakilishi wa  jimbo la kijito upele mh ali sleiman  ali shihata  na viongozi wa jimbo.

Amesema skuli hiyo bado inakabiliwa na uhaba wa vifaa na miundombinu isiyoridhisha hivyo kitendo hicho kinazidisha matatizo kwa walimu na wanafunzi wa skuli hiyo.

Nao viongozi hao wa jimbo wameahidi kukamilisha baadhi ya mahitaji muhimu kwa kujenga sehemu iliyobaki na baadae kuikabidhi wizara ya elimu kumalizia ujenzi huo.