UHAMASISHAJI WADAU WA SERIKALI ZA MITAA KUHUSU MRADI WA KUWAWEZESHA KIUCHUMI NA MAENDELEO

Taasisi mbali mbali zimeomba kuunga mkono malengo ya serikali ya kuwahudumia wananchi ili kurahisisha utendaji wa serikali za mitaa ili kuondoa kero zinazowakabili wananchi.
Mstahiki meya wa mji wa zanzibar khatib abdurahman khatib amesema kufanya hivyo kutasaidia maendeleo ya nchi haraka.
Akifungua mkutano wa uhamasishaji wadau wa serikali za mitaa kuhusu mradi wa kuwawezesha kiuchumi na maendeleo ya jamii engine amefahamisha kuwa ustawi wa nchi yoyote unahitaji kuimarishwa serikali za mitaa hivyo ni vyema kuweka mipango imara ya kufikia malengo yake.
Akitoa maelekezo kuhusu malengo makuu ya mradi huo mkufunzi wa mafunzo hayo tobiac celecele amesema mradi huo umeanzishwa ili kuiwezesha jamii kibiashara na kuwapatia mitaji ili kujikimu kimaisha baadhi ya yatendaji wamesema wanategemea mradi huo utasaidia kutoa fursa ya ajira kwa vijana hali itakayosaidia kundi hilo kuondokana na utegemezi