UHISPANIA YAANZISHA OPERESHENI KALI DHIDI YA UGAIDI

Hispania imeanzisha operesheni kali dhidi ya ugaidi, baada ya mshambuliaji anayedhaniwa ni mpiganaji wa itikadi kali kuvamia na lori eneo lenye watu wengi mjini barcelona, na kuua watu 13.
Katika operesheni hiyo watu watano walioshukiwa kutaka kufanya mashambulizi mengine wameuwawa na wengine kukamatwa ambao miongoni mwao ni raia kutoka morocco.
Kundi la dola ya kiislamu limedai kuhusika na shambulio hilo.
Mamlaka katika mkoa wa catalonia umeonya kwamba kuna mtuhumiwa aliyekuwa akipanga mashambulizi mengine mawili katika mji wa barcelona na mji mwingine maarufu ulioko pembezoni mwa bahari.