UHUSIANO MZURI KATI YA TANZANIA NA CHINA

 

Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh. Samia suluhu hassan amesema tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano mzuri kati ya tanzania na china kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande hizo mbili.

Akizungumza katika maadhimisho ya mwaka mpya wa kichina mh. Samia amesisitiza kuwa china imekuwa mshirikau mkubwa wa maendeleo tanzania kutokana na uhusiano huo.

Amemuhakikishia balozi wa china nchini dk. Lu youging kuwa serikali itaendelea kushirikiana na china katika kuimarisha sekta za biashara, utamaduni, elimu, afya  na masuala ya kijeshi kwa manufaa ya pande hizo.

Balozi wa china dkt lu youging amepongeza hatua zinachukuliwa na serikali ya tanzania katika kupambana na rushwa na ufisadi.

Amesema china inafurahishwa na hatua hizo zinazolenga kuimarisha utaji wa huduma bora kwa wananchi.

Katika maadhimisho hayo, balozi wa china nchini tanzania dkt  lu youging amemkabidhi makamu wa rais samia suluhu hassan mfano wa hundi ya shilingi milioni 70 fedha ambazo zitatumika katika ujenzi wa skuli ya msingi chato mkoani geita.