UJENGAJI HOLELA UNAOCHANGIA KUZIBWA NJIA ASILI ZA KUPITA MAJI

 

Mkuu wa wilaya ya kusini idrisa kitwana akemea ujengaji holela unaochangia kuzibwa njia asili za kupita maji msimu wa mvua na kunakosababisha maafa katika makaazi ya wananchi.

Akizungumza alipokuwa akiwatembelea waathirika wa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, amesema ni vyema wananchi kujali usalama wao kwenye maeneo ya makaazi ili kuepukana na hali hiyo.

Amewataka wananchi pamoja na masheha kuzingatia taratibu na sheria, pamoja kuahidi kuchukuliwa  hatua za haraka kwa waathirika  ili kudhibiti hali hiyo

Nao masheha wa  shehia tofauti wilayani humo, wameahidi kuwa makini zaidi katika kusimamia shughuli za ujenzi wa nyumba za makaazi .

Nao baadhi ya waathirika wa mvua hizo wameshauri kuchukuliwa hatua za haraka ili waweze kurudi katika maidha ya kawaida.

Kiasi nyumba 98 zimeathirika na mvua, huku nyumba 6 wakaazi wamelazimika kuhama katika nyumba zao.