UJENZI NA UKARABATI WA BARABARA PEMBA UTAWAWEWEESHA WANANCHI KUJIINUWA KIUCHUMI

 

 

 

 

 

 

Naibu waziri wa ujenzi mawasiliano na usafirishaji mh.mohammed ahmada salum amesema ujenzi  na ukarabati wa baadhi ya barabara kisiwani pemba  utawaweweesha  wananchi  katika kujienuwa kiuchumi kutokana na  kusafirisha mazao yao kurahisi.

Amesema  kwa sasa wizara  inaendelea   na jitihada zake za kuona ujenzi wa barabara hizo unamalizika kwa wakati  ili kuweza kutowa fursa kwa wananchi kwa kurahisishia usafiri.

Naibu waziri  huyo aliyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa  akizitembelea barabara hizo ikiwemo barabara ya ole –kengeja,mgagadu kiwani,kipapo-mgelema, kuyuni-ngomeni na barabara ya madenjani-mzambarauni ambayo barabara hiyo inafanyiwa ukarabati na kampuni  ya mecco kupitia fedha za ndani za mfuko wa barabara.

Naibu waziri huyo amemtaka msimamizi wa barabara  ya ole kengeja enginia amini khalid abdalla kusimamia vizuri mradi huo  ili wananchi waweze kufaidika na  barabara hiyo.

Akizungumzia ujenzi wa barabra ya ole kengeja inginia amini khalid amesema  watahakikisha  barabra hiyo  inakuwa yakiwango itakapomalizika  na itakayokidhi mahitaji  ya wananchi .

Nae meneja wa mradi  kutoka kampuni ya mecco nd,juma othman ambae  ni msimamizi wa ukarabati wa barabra ya madenjani –mzambarauni amesema katika ukarabati  huo  wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ya kuweko miundombinu ya maji  katika barabara hiyo huku akiwataka wananchi kuwa wastahamilivu  wakati  woete wa ukarabati wa barabara hiyo.

Pia naibu waziri wa ujenzi,mawasiliano na usafirishaji  mh,mohammed ahmada salum  amewataka wananchi  kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili  ya tarehe 2 mwezi wa nne  katika ufungunzi wa barabara  ya mgagadu –kiwani  ambapo katika ufungunzi huo  mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  rais wa zanzibar  na mwenyekiti wa barabara la mapindunzi zanzibar.