UJENZI WA BARABARA YA UNGUJA UKUU ILIYOATHIRIKA KWA MVUA

Naibu wa wizari ujenzi mawasiliano na usafirishaji mh mohamed ahmada amesema ameridhishwa na maandeleo ya ujenzi wa barabara ya unguja ukuu hali inayotia moyo kuanza kutumiwa na wananchi bila ya usumbufu katika kipindi kifupi kijecho.
Akizungumza alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi huo na barabara za mji wa zanzibar zilizoathirika na mvua za masika amesema hiyo ni miongoni mwa barabara zinazojengwa kwa ajili ya kuondoa kero za kijamii hasa katika suala la miundo mbinu bora.
Naibu waziri ahmada amefahamisha kuwa kwa sasa wanaendelea kuzifanyia matengenezo ya barabara za maeneo mbalimbali za mji wa zanzibar zilizoharibika kwa mvua ambapo kwa sasa wanandelea na ujenzi wa barara ya mchina mwanakwerekwe.
Mhandisi mtunzaji wa barabara idara ya ujenzi na utunzaji barabara cosmas masolwa ameelezea maaendeleo ya ujenzi wa barabara ya ungujaa ukuu huku akiwaomba wananchi kuunga mkono juhudi za utuinzaji wa barabara.
Wakati huo huo mw akilishi wa jimbo la bumbwini mh mtumwa pia ameshirikiana na wananchi katika uwekaji wa kifusi katika barabara ya panga tupu hadi bumbwini iliyoharibika katika kipindi cha mvua za masika ambapo amesema
Amesema lengo ni kuondosha kero hiyo katika hatua za awali wakati wakisubiri wizara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji kuifanyia matengenezo makubwa kama walivyoahidi.