UJENZI WA MTARO UNAOSIMAMIWA NA KAMPUNI YA CHINA YA CRJE.

 

Wananchi wa shehia ya  jangombe na migombani wamesifu hatua zinazoendelea kuchukuliwa  na serikali kupitia baraza la manispaa za  ujenzi wa mtaro unaosimamiwa na kampuni ya china ya crje.

Wakitoa  maoni yao wananchi hao wakati wakizungumza na zbc  kuhusu  hatua hiyo wamesema ni  mzuri  kwan kwa kiasi  inasaidiwa  kuondokana na  msongamano wa maji  kulingana na  siku za nyuma

Wamesema mbali na mafanikio hayo kumekuwa na matatizo ya kutuwama kwa maji kutokana na ardhi kuwa ya unyevu na wameiomba zawa kuufukia  mtaro  wa  kupitishia  maji  ambao unaweza kuleta madhara kwao na watoto wanaocheza katika maeneo hayo

Baadhi ya  mafundi wanaojenga mtaro huo wamewataka wananchi kuwa wastahamilivu  katika kufanikisha  ujenzi huo  na kuahidi kuukamilisha kwa wakati.

Wakizumgumzia matatizo wanayo kabiliana nayo ni kutopatiwa mikataba pamoja na ukosefu wa baadhi ya vifaa vya kufanyia kazi