UMUHIMU WA KUJENGA SKULI MPYA ZANZIBAR

Ujenzi wa skuli mpya katika mkoa wa mjini magharibi kumesababishwa na uwepo wa skuli nyingi zanzibar zenye mrundikano wa wanafunzi katika darasa moja jambo linalohatarisha hata usalama wa kiafya kwa wanafunzi.
Zbc imetembelea baadhi ya skuli zinazojengwa na kuona hatua mbalimbali za ujenzi huo ukiendelea ikiwemo skuli ya muembeshauri na chumbuni.
Akizungumza na zbc afisa elimu mkoa wa mjini magharib mw.khatib tabia amesema kuna umuhimu mkubwa wa kujenga skuli hizo kwani zitasaidia kupata afya njema wanafunzi pamoja na ufahamu mzuri kutokana na kusoma katika hali ya idadi ya wastan ya wanafunzi katika madarasa hayo.
Akielezea suala la uwepo wa walimu wa kutosha katika skuli hizo mpya, mw.khatib amesema serikali ina vyuo vingi vinavotoa zaidi ya asilimia sabini ya wataalamu wa fani hiyo,hivyo wizara imejipanga vyema kuwatumia walimu hao.
Skuli hizo tisa zinatarajiwa kujengwa unguja na pemba zikiwa ni pamoja na skuli ya mwembeshauri, kinuni,chumbuni,bububu na fuoni kwa mkoa wa mjini magharib unguja zitajengwa kwa mkopo wa shirika la mafuta la opek la afrika.