UJIO WA VIONGOZI WA FIFA NA CAF WANATARAJIA KUWASILI NCHINI

 

Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo mhe dkt harison mwakyembe amekutana na wahariri wa habari za michezo wa vyombo mbalimbali nchini  kuzungumzia  ujio wa viongozi wa fifa na caf wanatarajia kuwasili nchini tarehe 21 hadi tarehe 22 februari mwaka huu kwa ajili ya  kufanya mkutana wao  

Akizunguza na wahariri hao katika uwanja wa uhuru dar-es-salaam waziri mwakyembe amesema  seriakali kwa kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu (tff) wameona ni vyema kukutana ili kubadilishana mawazo juu ya namna ya kupokea ugeni huo  mkubwa kwani tanzania ina sifa ya kupokea wageni kwa ukarimu.

Naye rais wa shirikisho la mpira wa miguu tanzania tff ndugu wallace karia amewataka wanahabari kutanguliza mbele maslahi ya taifa na kutojihusisha na maswali yanayoihusu zanzibar kwa kuwa tayari suala la zfa limekuwa likishughulikiwa.