UJUMBE WA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA UMEWASILI NCHINI BANGLADESH

 

Ujumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa umewasili nchini bangladesh  kushuhudia maafa yanayowakabili wakimbizi 700,000 wa jamii ya rohingya kutoka myanmar waliokimbia ukatili wanaofanyiwa na jeshi la nchi hiyo wakitafuta hifadhi ya umoja wa mataifa ili warudi nyumbani .

timu hiyo itakutana na baadhi ya wakimbizi, ambao baadhi yao walibakwa na kuteswa ambapo  ujumbe huo wa umoja wa mataifa utaelekea nchini myanmar jumatatu hii.

vikosi vya usalama vya myanmar vinashutumiwa kwa ubakaji, mauaji, mateso na kuchoma moto nyumba za warohingya huku  maelfu wakiaminika kuwa wameuawa.

vurugu za hivi karibuni Nchini Myanmar zilianza wakati waasi wa kirohingya walipofanya mfululizo wa mashambulizi agosti 25 dhidi ya vituo 30 vya usalama pamoja na maeneo mengine.