UJUMBE WA WATU 10 KUTOKA SERIKALI YA MJI WA ZHONGLOU KATIKA JIMBO LA CHANGZHOU NCHINI CHINA UMEFANYA MAZUNGUMZO

Ujumbe wa watu kumi kutoka Serikali ya mji wa zhonglou katika jimbo la Changzhou nchini China umefanya mazungumzo na mawaziri pamoja na watendaji wa juu wa Serikali kuhusu maeneo mbalimbali wanayoweza kushirikiana na Zanzibar.

Waziri wa Biashara, Viwanda na masoko Balozi amina salum ali ambae alikuwa mwenyeji wa mkutano huo ameuambia ujumbe huo kuwa zanzibar imetenga eneo kubwa la kuwekeza hivyo ameuomba uongozi huo kuangalia maeneo gani ambayo wanaweza kushirikiana na zanzibar kwa manufaa ya pande mbili.

amesema sekta ya afya pia inahitaji ushirikiano kama ilivyofanywa kwa Hospitali ya Abdalla mzee ambapo serikali ya china imetoa msaada mkubwa katika kuiimarisha.

Naibu Meya wa mji wa Zhonglu Han Jun ameahidi kuwa watashirikiana katika nyanja mbalimbali ili kukuza uhusiano kati ya china na Zanzibar katika kukuza maendeleo.

mkutano huo umehusisha karibu wizara tisa za Serikali Ya Mapinduzi Zanzibar, pamoja na taasisi na taasisi zake ikiwemo mamlaka ya vitenga uchumi zipa.