UKAGUZI KATIKA SKULI YA TRIFONIA ACADEMY NA KUGUNDUWA MAPUNGUFU KADHAA

Uongozi wa baraza la manispaa ya magharibi b imefanya ukaguzi katika skuli ya trifonia academy na kugunduwa mapungufu kadhaa ambayo hayaridhishi kwa usalama na afya za wanafunzi.
Ukaguzi huo uliongozwa na murugenzi wa manispaa hiyo amour ali mussa umefanyika kwa maeneo ya dakhalia ambapo imegundulika kuwa kuna mrundikano wa wanafunzi katika vyumba vya kulala hali inayotishia usalama wao hasa katika suala zima la uvutaji wa hewa na mwanga mdogo.
Wamesema pia kumekuwa na mchanganyiko katika vyumba vya kulala kwa kuwachanganya wanafunzi wakubwa na wadogo hali inayoweza ikawa chanzo cha kufanyika vitendo viouvu na ikatoa muda wa wiki moja kwa uongozi wa skuli hiyo kurekebisha mapungufu hayo au wataichukulia hatua ikiwemo kufungiwa.
Wanafunzi wa skuli ya trifonia wamesema hali hiyo sio nzuri kwani hupata shida wakati wa joto na baridi kwavile vyumba vyao havina dari na kuvujisha wakati wa mvua huku uongozi wa skuli ukiaahidi kufanya marekebisho ndani ya muda waliopewa.
Hii ni mara ya pili kwa skuli ya trifonia academy kufanyiwa ukaguzi na baraza la manispaa katika kipindi cha takriban mwezi mmoja na kugundua kasoro hizo na hawajazirekebisha.