UKARABATI WA MADARASA NA VYOO KATIKA SKULI YA MAANDALIZI KIDUTANI

 

Mkuu wa mkoa mjini magharib  mh.ayubu mohamedi mahamod  ameahidi kusaidia  ukarabati wa madarasa na vyoo katika skuli ya maandalizi kidutani  ili kuwapatia wanafunzi elimu bora inayotolewa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar.

Amesema hayo wakati wa siku ya wazazi  huko katika skili ya maandalizi kidutani.

Amesema walimu wana kazi kubwa  katika kuwaanda wanafunzi  katika maandalizi  kuelekea msingi kwa kuwafundisha vipaji mbali mbali

Naye mwenyekiti wa kamati hiyo  bwana ameri hamza amewaomba wazazi  wa wanafuzi hao kuja kuwachukua mapema  ili kujiepusha na vitendo viovu.

kwa upanda wa mkurugenzi  ya skuli ya maandalizi na msingi   bibi safia  ali  rijali  amesema  hisa sasa  serikali imejipanga kuinua kiwango kizuri  kwa  kuwapatia elimu bora   na yenye viwango