UKOSEFU WA AJIRA LITAPUNGUA KUPITIA MKAKATI WA KUTOA MIKOPO YA MARA KWA MARA KA VIJANA.

 

Waziri wa Kazi, uwezeshaji Wazee, Vijana, Wanawake na watoto Mh. Modline Castico amesema zaidi ya mikopo 300 imetolewa kwa mwaka 2016/2017.

amesema mikopo hiyo ni kwa unguja na pemba ambapo wizara inamatumaini makubwa itawasaidia vijana  kujiendeleza katika masuala mbali mbali ya kujiajiri.

akitoa taarifa  kwa waandishi wa habari katika madhimisho ya siku ya vijana kimataifa, amesema mikopo hiyo imewalenga vijana wa makundi mbalimbali na lengo kuu ni kuweza kunufaika nayo, na kutaja watu wenye ulemavu na vijana  wenye umri wa mika 18 -35 kuwa ndio asilimia kubwa iliyotakiwa.

amesema serikali inafahamu kwamba vijana ndio nguvu kazi ya taifa na tatizo la ukosefu wa ajira litapungua kupitia mkakati wa kutoa mikopo ya mara kwa mara ka vijana.

hata hivyo mh. castico amewataka vijana kuendelea kudumisha amani  iliyopo nchini na kuwashajihisha kujiajiri wenyewe katika nyanja mbalimbali za kiuchumi kwa kuitumia vizuri fursa ya upatikanaji wa mikopo hiyo.