UKOSEFU WA ELIMU YA KUMBUKUMBU KWA BAADHI YA WATENDAJI

 

Kumbukumbu nyingi katika ngazi ya shehia zimekosa kuhifadhiwa vizuri kutokana na ama kwa kutokujua kunakosababishwa na ukosefu wa elimu ya kumbukumbu kwa baadhi ya watendaji.

Taasisi ya nyaraka na kumbukumbu zanzibar ikiwa katika muendelezo wa mafunzo kwa masheha wa wilaya za zanzibar, imesema kuna kumbukumbu nyingi zinazozalishwa katika shehia lakini uhifadhi w ake bado haukidhi vigezo na kusababisha kukosekana.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo akizungumza na masheha wa wilaya ya magharib a katika mafunzo ya utunzani na usimamizi wa kumbukumbu amesema taasisi katika kusimmaia suala hilo imependekeza majengo yote ya serikali yawe na vyumba vya kuhifadhi kumbukumbu kwa faida ya vizazi vilivyopo na vinavyokuja.

Wakitoa maoni yao baadhi ya masheha wamesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kutambua thamni ya kutunza kumbukumbu kwani wao ni kiungo muhimu katika kukusanya taarifa za awali zinazohusu masuala mbalimbali ya kijamii.

Mkuu wa wilaya ya magharibi a kepten khatib khamis amehimiza uaminifu na utunzaji mzuri wa kumbukumbu kwani zinasaidia katika shughuli za maendeleo  na kutolea uamuzi kwa baadhi ya mambo.