UKOSEFU WA MITAJI NI CHANGAMOTO ZINAZOZIKABILI SACCOS

 

 

Ukosefu  wa  mitaji  ya kutosha  ni   changamoto  zinazozikabili saccos  nyingi na kuchangia  kufa  au  kutoimarisha  biashara zao  kwa kutofikia  malengo.

Wakibainisha  changamoto zinazowakwaza  wanasaccos  wa  uvivini na  mtakuja    zilizopo   tumbatu   wamesema   ufinyu  wa  fedha  unakwamisha  utekelezaji wa  harakati  zao  zinazochangia kupambana  na  ukali  wa  maisha  vijijini  mwao.

Sheha  wa shehia  ya  uvivini  nd hassan  mwadini  amesema  saccos  zilizopo  katika  shehia  hiyo  zinahitaji   kupatiwa  taaluma  ili   zijiendeshe  kibiashara  kama   ni  njia  ya  kujiongezea   kipato    kutokana na  miradi  yao.

Mbunde wa  jimbo  hilo  mh  juma  othman  hija  katika  kuzikagua  saccos  hizo  amewashauri kuwa  karibu  na  viongozi  wa jimbo  katika  kuharakisha   maendeleo  jimboni mwao