UKUSANYAJI WA MAPATO KATIKA VIANZIO VYA NDANI 2017-2018

Manispaa ya Magharib A imekusudia kuimarisha ukusanyaji wa mapato katika vianzio vya ndani ili kupiga hatua katika makadirio ya mapato ya mwaka 2017-2018.
Akiwasilisha ripoti ya makadirio ya makusanyo katika mwaka wa fedha 2017-2018 katika kikao cha bajeti cha madiwani wa manispaa hiyo, mkurugenzi wa manispaa ya Magharib A Said Juma amesema baraza linakadiria kukusanya shillingi billioni moja, milllion mia nne na hamsini na moja ambazo ni pamoja na makusanyo ya ndani,fedha kutoka taasisi zilizogatuliwa na fedha za ruzuku kutoka serikali kuu.
Aidha mkurugenzi huyo amesema hatua zitakazoimarishwa ili kufikia makadirio ya shillingi milioni mia sita na hamsini kwa makusanyo ya ndani,ni pamoja na kuvifanyia mapitio viwango vya ada, kodi na tozo mbalimbali ili viendane na mazingira halisi yaliyopo katika utoaji wa huduma na kuingia katika mfumo wa kielektronik wa ukusanyaji wa mapato.
Wakitoa micha ngo madiwani wa manispaa hiyo wamesema katika kufanikisha mpango huo wataendelea kufanyakazi kwa ufanisi na wananchi watarajie mafanikio zaidi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa baraza hilo ambae ni mea wa manispaa ya magharib a hamza khamis juma amewataka madiwani kuwa makini katika kusimamia changamoto zilizopo ndani ya manispaa hiyo zikiwemo uchafuzi wa mazingira na uvamizi wa maeneo ya wazi.