ULINZI NA USALAMA KATIKA MAENEO YA WELEZO

Naibu waziri wa mambo ya ndani wa serikali ya jamhuri ya muungano mh. Hamadui yussuf masauni ameliagiza jeshi la polisi kwa muda wa wiki mbili kuhakikisha ulinzi na usalama katika maeneo ya welezo miembe saba na mwanyanya mkoroshoni unaimarika vizuri ili kukabiliana na vitendo vya kihalifu.
Agizo hilo amelitoa nyakati tofauti baada ya kukagua maeneo hayo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa kukithiri vitendo vya uhalifu na kusema kuwa hawezi kuona wananchi wakiishi katika maisha ya hofu na kushindwa kufanya shughuli zao za kijamii.
Mh masauni amesema nchi hawezi kwenda kama hakuna serikali wala jeshi la polisi na kushangazwa kuona watu wanapigwa na kunyang’anywa vitu vyao huku akilisisitiza jeshi hilo kuwakamata wote wanaohusika na vitendo hivyo kwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Wakitoa malalamiko yao wakaazi wa welezo na mwanyanya wamesema wamekuwa na hofu juu ya usalama wao kutokana kutokezea baadhi ya watu ambao kuwashabulia kwa silaha za kienyeji na kuwaibia vityu vyao huku wakishauri kujengewa kituo cha polisi katika maeneo yao.
Mkuu wa upelelezi wilaya ya mgharib a, asp suleiman khamis akitoa maelezo yake amesema wamefanikiwa kuwakamata baadhi ya wahalifu ambao wamekuwa ni tishio katika wilaya hiyo.