UMEFIKA WAKATI KWA VIJANA KUZITUMIA ARDHI ZILIZOPO KWA KILIMO ILI KUONDOKANA NA UTEGEMEZI

 

Rais  mstaafu wa  jamhuri ya muungano  ya  tanzania mh  ali  hassan  mwinyi  amesema umefika wakati kwa  vijana  kuzitumia ardhi  zilizopo  katika  kujihusisha na kilimo  ili  kuondokana na utegemezi na  kujitosheleza  kwa  chakula nchini.

Akizungumza na waandishi wa  habari   alipokuwa katika  shambalake  analolima  mipapai lililopo  kitope  amesema ni vyema kujiwekeza  zaidi katika  masuala  ya  kilimo  ili  kuweza  kujikimu  kimaisha  na  kuachana na vikundi  vyenye  kuwashajihisha na   vitendo  viovu  visivyo na  tija  kwao  na  taifa  kwa  ujumla.

Amefahamisha kuwa iwapo  watajikita  zaidi katika  kilimo  cha  kitaalamu   kitachowawezesha  kuvuna kwa  muda  mfupi  ili  waweze  kuendesha  maisha  yao na kunyanyua  uchumi  wa nchi.

Akizungumzia  kilimo  hicho  cha  mipapai  mh  mwinyi  amesema  kina  tija  iwapo  watakilima  kwa  kufuata  maelekezo  ya  kitaalamu sambamba na  kuimarisha miundombinu  ya umwagiliaji  wa  kisasa  kwa  maji  ya  matone.

Mtaalamu  wa  kilimo  hicho kutoka  egypt   dr.reda  abdalla  abdelaziz  amesema  iwapo  wakulima  watapokea  ushauri   ipasavyo  juu  ya  kilimo  hicho wataweza  kumudu  udhibiti wa  soko  hilo  na kujinyanyua  kiuchumi.

Nae  mlinzi  mkuu wa  shamba  hilo ali simai  mwita amesema   hali  ya  shamba  hilo  iko  vizuri  ila  wanapambana  na  wanyama kutokana  na  uharibifu  wa  mazao  yaliopo  shambani.

Shamba  hilo  lenye  jumla  ya ekari  5  limelimwa  mipapai yenye  kuzingatia  kilimo  cha  kisasa  lina  miezi 5 sasa  baada  miezi 2  yanatarajiwa  kuvunwa   kwa kila muda wa siku 3 hadi 5  huku  mpapai  mmoja  unabeba  mapapai  30  hadi  50 kwa  muda wa  miaka 2.