UMEFIKA WAKATI KWA WAKULIMA KUPATIWA ELIMU SAHIHI JUU YA BIDHAA WANAZOZIZALISHA

 

 

Umefika  wakati  kwa  wakulima  kupatiwa  elimu  sahihi  juu  ya  bidhaa  wanazozizalisha ili  ziweze  kuwa  ni  nyenzo  inayowawezesha  kumudu  harakati  zao  za kimaisha.

Hayo  yamebainishwa  na  wataalamu  wa  kilimo  kutoka  taasisi kilele  inayohamasisha ukulima wa  mboga mboga  na  matunda  taha  walipokuwa  wakielekeza  wakulima  walipolitembelea shamba  la  mfano  la   mkulima  salum  kamshuu  lilipo  hanyegwa  mchana.

Wataalamu  hao  wamesema ni  wakati  sasa  wakulima  wa  kukubali  mabadiliko  ili kuweza  kuvuna  kwa  wingi  katika  eneo  dogo  kwa  kufuata utaratibu  huku  wakizingatia kalenda ya  ukulima  ili  kuendana  na  mahitaji  ya  soko  la  bidhaa  wanazozizalisha.

Wakulima  walitembelea  shamba  hilo  kwa  kupatiwa  taaluma  juu  ya  kilimo  cha  mboga  mboga   wameishauri  serikali  kupitia wizara  kazi  uwezeshaji  wazee  wanawake  na  watoto   kuwapatia  mikopo  isio  na  riba  sambamba  na  kuwatofautisha  na  wafanyabiashara  kutokana  na kipato  chao  cha  msimu  wanachokizalisha.

Shamba  hilo  lenye  jumla  ya  ekari  moja  na  robo  limeanza  kulimwa tungule  kitaalamu  kwa  kutumia  mbegu  ya  spiner chini  ushauri  na  maelekezo  ya  jumuiya  ya  taha  mnamo  mwezi  wa  nane ambalo  linakadiriwa  kuvuna  zaidi  tani 25.