UMOJA WA MATAIFA WAUNGA MKONO VIKWAZO VIPYA DHIDI YA KOREA KASKAZINI

Baraza la usalama la umoja wa mataifa, limeunga mkono vikwazo vipya dhidi ya korea kaskazini baada ya kuifanyia majaribio zana zake kinyukilia wiki ya iliyopita.
Katika kura ya pamoja, baraza hilo limeidhinisha vikwazo hivyo vipya, vinavyolenga biashara ya chuma na mkaa ya mawe zinazouzwa na nchi hiyo nje kwa zaidi ya dola bilioni kwa mwaka.
Rais wa marekani donald trump, amepongeza hatua za china na urusi za kuunga mkono vikwazo hivyo vilivyotolewa na baraza hilo la umoja wa mataifa huku korea kusini, wameiomba korea kaskazini kurejea katika mazungumzo, ili kutatua mzozo wa mpango wake wa zana za kinuklia.