UMUHIMU WA KUENDELEZWA VIJANA WANAOSOMA FANI YA UFUNDI

bodi ya kusajili wakandarasi imesema kuna umuhimu wa kuendelezwa vijana wanaosoma fani mbalimbali za ufundi ili kuwajenga kitaaluma zaidi.
mrajis wa bodi ya usajili wakandarasi talha masoud ali amesema juhudi hizo zitafanikisha kuongeza idadi ya wataalamu hasa wakandarasi wazalendo wanaohitajika kwa kiwango kikubwa zanzibar.
akizungumza wakati akikabidhi vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya shilingi milioni 12 kwa skuli ya sekondari na ufundi lumumba na kengeja zanzibar amesema msaada huo ni juhudi za kufanikisha ufundishaji bora ambapo kwa sasa kuna mwamko mdogo.
walimu wa skuli hizo zilizokabidhiwa vifaa na mkurugenzi elimu sekondari bi asya iddi issa wameomba wadau mbalimbali kuziendeleza skulihizo kwa vifaa na hata walimu wake kupewa mafunzo zaidi. wakati huhuo bodi hiyo imetoa zawadi kwa wanafunzi wa kidato cha nne wa skuli mbalimbali za zanzibar waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi katika mitihani yao ya taifa amesema bado mwamko mdogo wa masomo ya sayansi hivyo mpango wa kutoa zawadi utasaidia kuyapa umuhimu masomo hayo.
baadhi ya wanafunzi wameahidi kuendelea na masomo yao ili kuweza kujiari katika fani ya uhandisi ili kuchangia kukua kwa uchumi wa nchi .
zaidi ya wanafunzi sabini wa skuli za sekondari zanzibar wamepatiwa vyeti na fedha taslim ambapo skuli ya sekondari lumumba imefanikiwa kupata nafasi ya kwanza katika masomo ya sayansi kwa upande wa zanzibar