UMUHIMU WA KUWALEA WATOTO KATIKA MALEZI BORA

 

 

Mke wa Rais wa Zanzibar  Mama  Mwanamwema Shein  amesisitiza umuhimu wa kuwalea watoto katika malezi bora ili jamii iweze kuwa  na watu wenye maadili.

Katika kutimiza jukumu hilo amehimiza ushirikiano katika kulea watoto kwa pamoja  kwani jukumu hilo si la mtu mmoja  pekee bali jamii nzima ishiriki katika suala hilo.

Mama shein alikuwa akizungumza wakati akiwatunuku pete za dhahabu akina mama wa sos tanzania bara na zanzibar wanaofanya kazi ya kuwalea watoto katika taasisi ya sos na kusema kuwa serikali inatekeleza jukumu lake kwa kusaidia mambo mbalimbali ili kuwajengea ustawi mzuri wa maisha yao.

Mama mwana mwema shein pia amekemea tabia ya baadhi ya watu kuwafanyia watoto vitendo vya ukatili na udhalilishaji jambo linalokwenda kinyume na maadili na uvunjidu wa haki za binadamu.

Kwa upande wake naibu waziri wa kazi uwezeshaji wazee vijana wanawake na wototo mh shadya mohammed amewapongeza akina mama hao kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kuwalea wtoto hao.

Rais wa taasisi ya sos duniani sidhartha kaul kwa malezi wanayopatiwa watoto ambao wanalelewa katik vijiji vya sos na kusema kuwa jambo hilo linahitaji moyo.