UN KUSHIRIKIANA NA GAMBIA

Umoja wa mataifa umetangaza kuwa, uko tayari kushirikiana na serikali mpya ya gambia katika masuala ya kimahakama na haki za binadamu.
Katika mazungumzo yake na rais wa gambia adama barrow, mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa akiwa safarini nchini humo amesisitiza kuweko maridhiano ya kitaifa baina ya makundi ya kisiasa ya nchi hiyo na kutekelezwa uadilifu kuhusiana na watenda jinai.
Siku chache zilizopita, shirika la kutetea haki za binadamu la human rights watch lilitoa ripoti iliyoeleza kwamba, serikali ya jammeh ilikuwa ikitumia vitisho na utesaji dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani pamoja na kuwanyima haki zao za msingi.