UONGOZI WA BARAZA LA MJI WETE UMEFANIKIWA KUKUSANYA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 60

 

Uongozi wa baraza la mji wete umefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 60, kutoka kwenye vyanzo vyake mbali mbali vya mapato kwa kipindi cha kuanzia mwezi julai hadi septemba mwaka 2018.

Hayo yameelezwa na   mhasibu wa baraza hilo Ali Khafan Haji kwenye kikao cha kujadili mapato na matumizi ya baraza kwa  mwezi wa julai – septemba 2018.

amesema  awali baraza walikadiria kukusanya  shili milion 61 kwa kipindi  hicho , lakini kutokana na mwitikio wa wafanyabiashara wa kupia kodi wameweza kuvuka lengo walilokusudia.

akitoa maelezo juu ya mafanikio hayo  mkurugenzi wa baraza hilo hamadi mbwana shehe amesema kutokana na juhudi kubwa iliochukuliwa juu ya kuvisimamia vyanzo vya mapato ndio iliopelekea kupatikana kwa mapato hayo.

Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya wete bi  mkufu faki ali ameupongeza uongozi wa baraza la mji wete ,kwa juhudi zake walizochukua hadi kufanikisha kupata zaidi ya mafanikio walioyakusudia.