UONGOZI WA CHUMBUNI UMESEMA UTAISHAWISHI SERIKALI KUSAIDIA KUANZISHA MRADI WA SKLULI YA SEKONDARI

 

 

Uongozi wa jimbo la chumbuni umesema utaishawishi serikali kusaidia kuanzisha mradi wa skluli ya sekondari katika jimbo hilo kutokana na wanafunzi wengi kufuata elimu katika skuli zilizopo nje ya jimbo hilo.Mbunge wa jimbo la chumbuni ussi salum pondeza akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya ccm kwa upande wake katika mkutano wa kamati amesema masuala mengi muhimu ya kijamii yametekelezwa jimboni humo ikiwemo kuimarisha hospitali lakini kipaumbele chengine muhimu ni kuimarisha sekta ya elimu.

Amesema ametumia zaidi ya shilingi milioni mia mbili na 17 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwa ni kutekeleza kwa vitendo ilani ya chama.Viongozi wengine    wa jimbo wakiwemo madiwani wamewaslisha taarifa zao za utekelezaji kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi januari hadi disemba 2017 zikugisia zaidi utekelezaji wa miradi ya usafi na mazingira.