UONGOZI WA HOSPITALI YA KIMATAIFA YA MIOT YA JIMBO LA CHENNAI NCHINI INDIA UMEAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA ZANZIBAR KATIKA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA

Uongozi wa hospitali ya kimataifa ya miot ya jimbo la chennai nchini india umeahidi kuendelea kushirikiana na zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinawafikia wananchi  wote wa zanzibar.

Kauli hiyo imetolewa na mmiliki wa hospitali hiyo dr. Mahandazaz katika  mazungumzo yake na makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi na ujumbe wake waliofika kukagua wagonjwa wa wanaogharamiwa matibabu na serikali ya mapinduzi ya zanzibar.

Dr.mahandazaz  amesema mkataba uliotiwa saini hivi karibuni kati ya
hospitali hiyo na wizara ya afya ya zanzibar ni mwanzo wa safari ndefu ya matumaini inayoashiria ushirikiano mwema utakaoleta faraja kwa wagonjwa wote kitanzania waopangiwa kupata huduma za afya kwenye taasisi hiyo.

Alisema yapo mambo mengi ambayo miot imekusudia kuyatekeleza katika kipindi kifupi kijacho likiwemo suala la kupatiwa mafunzo kwa
madaktari na baadhi ya wataalamu wa afya wa zanzibar lengo likiwa
kuwajengea uwezo wa kutoa huduma za afya zinazokusudiwa kupatikanakatika kiwango cha kimataifa.

Dr. Mahandazaz alimuhakikishia makamu wa pili wa rais wa zanzibar naujumbe wake uliomo nchini india kwa ziara ya wiki moja kwamba
hospitali hiyo itaendelea kuwahudumia wagonjwa wa kitanzania wakatiwowote wanapoamuliwa kupelekwa katika taasisi hiyo kwa ajili ya kupata huduma za afya.

Naye katibu mkuu wizara ya afya zanzibar bibi asha ali abdulla
ameushuruku uongozi na madaktari wa hospitali ya miot jimboni chennai kwa jitihada wanazochukuwa za kuwapatia huduma za afya wagonjwa wa kitanzania wanaofikishwa kwenye hospitali hiyo.
Bibi asha alisema inaleta faraja na kuona zaidi ya wagonjwa 171 wa
zanzibar tayari wameshapatiwa huduma za afya zikiwemo operesheni za maradhi mbali mbali baina ya mwaka 2012 hadi 2015.
Alisema katika kupunguza idadi ya wagonjwa na gharama zake za
kupelekwa nje ya nchi wananchi wanaopatwa na matatizo makubwa ya kiafya serikali ya mapinduzi ya zanzibar kupitia wizara ya afya
inaendelea kuimarisha huduma za afya katika hatua ya kuwa na hospitali za rufaa.

Makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif  na ujumbe wake alipata wasaa wa kutembelea vitengo mbali mbali vya hospitali hiyo ya miot ili kujionea uwajibikaji wa watendaji wake na baadae kukagua baadhi ya wagonjwa wa kitanzania waliolazwa kwa ajili ya kupata huduma za afya ziliwemo operesheni.
Akielezea faraja wanayoipata kutokana na huduma zinazotolewa kwenye hospitali hiyo mzazi wa mgonjwa hemed hafidh anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili baba hafidh hemed suleiman kwa niaba ya wagonjwa wa kitanzania ameishukuru serikali ya mapinduzi ya zanzibar  kwa moyo thabiti  inayoonyesha wa kugharamia matibabu ya wananchi wake.

Baba hafidh alimthibitishia balozi seif  na ujumbe wake kwamba
wagonjwa wa zanzibar hadi sasa ndio pekee wanaogharamiwa  na serikali ya mapinduzi ya zanzibar huduma za matibabu wakati wanapopekekwa katika hospitali hiyo.

Makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif na ujumbe wake
atamalizia ziara yake ya siku tano katika mji wa new delhi kwa
kutembelea kiwanda cha matrekta cha mahindra, kukutana kwa mazungumzo na wafanyabiashara pamoja na wawekezaji wa india.