UONGOZI WA KITUO CHA AZAM KUANDAA VIPINDI VINAVYOHUSIANA NA MAMBO YA KALE

 

 

Waziri wa habari utamaduni na mambo ya kale mh.mahmoud thabit kombo ameushauri uongozi wa kituo cha matangazo cha azam kuandaa vipindi vinavyohusiana na mambo ya kale ili kutoa elimu kwa wananchi wapate kutambua tamaduni zao.Akizungumza na baada ya kutembelea wizara ya habari utamaduni na mambo ya kale na shirika la utangazaji zanzibar zbc ,.mh.mahmud amesema kufanyika kwa vipindi hivyo kutasaidia kuutangaza utamaduni kuwahamasisha watazamaji.

nae mkurugenzi mtendaji wa azam bw.tido muhando amesema wanauthamini uhusiano wao na zbc kwani watajifunza mengi zanzibar lakini pia ni chachu ya maendeleo kwa wafanyakazi wa pande zote kwa kuwajengea msingi mzuri wa uimara kwa vitendo katika kuboresha ufanisi kwenye kazi.Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la zbc bi aiman duwe amesema pamoja na mafanikio ya studio mpya yaliyopatikana bado upo umuhimu mkubwa kwa wafanyakazi kupatiwa elimu zaidi juu ya matumizi ya vifaa vipya  na kurudisha hadhi ta tv ya kwanza ya rangi afrika mashariki.