UPANDAJI MITI ILI KUIMARISHA MAZINGIRA

Wananchi wamesisitizwa kushiriki katika upandaji miti ili kuimarisha mazingira katika kukabiliana na mabadiliko y a tabia nchi.
Mratibu wa mradi wa kuhamasisha upandaji miti wa root and shoot Japhet Mwanang’ombe amesema mabadiliko ya hali ya hewa yanahitaji kukabailiwa ili kuepusha nchi kuwa na jangwa.
Akizungumza katika upandaji miti ya mikoko katika maeneo ya fukwe za bububu ameshauri shughuli za upandaji miti kuwekwa kipaumbele kuanzia ngazi ya shehia ili kuongeza mwamko wa jamii
Afisa wizara ya kilimo omar hakim na mratibu wa club za mazingira mwalimu Ame Haji Vuai wamesema wamepanda miti hiyo ili kurejesha uhalisia maeneo yalioathirika na mmong’onyoko wa ardhi kando ya fukwe za eneo hilo la Bububu.