UPEPO MKUBWA UMEANGUSHA MITI NA KUHARIBU NYUMBA

Upepo mkubwa usio wa kawaida  umeangusha  miti na  kuharibu nyumba za  takribani  15  maeneo ya ndijani muembe  punda  na dunga kiembeni.

Upepo   huo  uliovuma  majira  ya  mchana   hapo   jana  umesababisha  hasara  kubwa  pamoja  na  kubomoa  skuli  ya  maandalizi   dunga  kufuatia    kuangukiwa  na  mnazi  ambapo

mtu   mmoja   amejeruhiwa  baada   ya  kuangukiwa  na   tawi   la   muembe

Mashuhuda  wa   tuko  hilo   wamesema  upepo  huo  ulikuwa  na   kasi   ya   ajabu  ambayo   hawajawahi   kuiona   katika   siku  za   karibuni   na  kuwataka  wakaazi  kuchukua   tahadhari   wakati   wote

Viongozio wa  mkoa kusini unguja wamefika maemeo yaliyoathiriwa na upepo huo uu wa wilaya ya kati nd. Mashavu sukwa, na mkuu wa kusini unguja dr. Idrissa muslim hijja  wakiangalia maafa hayo na kuwafariji wahanga wa upepo huo   na  uliyovuma kwa wastani wa nusu saa jana mchana wamesema   nyumba 16 ikiwemo skuli ya maandalizi ya ndijani mwembe punda zimeathirika na  upepo huo  uliongoa  na kukata miti mbalimbali  ikiwemo miembe na minazi.

Wakaazi wa maeneo hayo walio kuepo eneo hilo la upepo  wamesema tawi moja la muwembe limevuruga kibanda cha bi. Mariyam kashindia aliyekuwemo ndani na kuumia vibaya pamoja na kuizua  mapaa  ya  nyumba  mbalimbali.