UPOTEVU MKUBWA WA MAFUTA YA MIMEA YA MKARATUSI

 

Muwekezaji kutoka kampuni ya kunshan asia orama ltd ya china zhou junxue amesema kuna upotevu mkubwa wa mafuta ya mimea ya mkaratusi yanayozalishwa katika kiwanda cha mtakata wawi vinavyomilikiwa na shirika la zstc.

Junxue ambae ni mwenyekiti wa kampuni KUNSHAN ametowa kauli hiyo baada ya kutembelea kiwanda cha kuzalishia mafuta ya mimea Mtakata, kiwanda cha Makonyo na eneo linalotarajiwa kupandwa mikaratusi Micheweni.

Amesema amegunduwa kuwa katika uzalishaji huo ni majani pekee ndio yanayokamuliwa mafuta na matawi kufanywa kuni kitendo ambacho si utaalamu katika uzalishaji huo.

Katika hutua nyengine Junxue amesema baada ya kupandwa kwa miti hiyo, wakati wa kuvuna ataleta wataalamu ambao watawafahamisha namna ya kuvuna na vipi maji na matawi watayazalisha mafuta hayo.

Akikagua eneo la linalotarajiwa kupandwa mikaratusi Junxue amehakikishiwa na Mkuu wa wilaya ya Micheweni Nd. Salama Mbarouk Khatib kwamba wanayo maeneo ya kutosha ya uwekezaji na vijana wako tayari kufanya kazi hiyo.

Akitembelea kiwanda cha mafuta ya makonyo na mimea mwenyekiti Junxue akiwa amefuatana na uongozi wa wizara ya Viwanda Biashara na Masoko amesema alichokigundua ni kuwepo kwa mitambo iliyochakaa ambayo haina uwezo wa kuzalisha bidhaa kwa wingi.