UPUNGUFU WA DAMU SALAMA NCHINI AMBAO WAKATI MWENGINE HULETA ATHARI.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema wakati umefika kwa kila mwananchi mwenye sifa za uchangiaji damu kujitolea ili kuiepusha jamii kukumbwa na upungufu wa damu salama nchini ambao wakati mwengine huleta athari.

Amesema upungufu mkubwa wa damu ulijitokeza mwaka uliopita hasa katika kipindi mwezi mtukufu wa ramadhani kwa mujibu wa takwimu katika maabara za hospitali zanzibar na kusababisha kuomba msaada akizungumza katika Bonaza la Uchangiaji Damu Salama lililoandaliwa na Mkoa wa Kusini Unguja na kufanyika Dunga Wilaya ya Kati Balozi Seif Ali Iddi alisema kwa mujibu wa Takwimu zilizopo inaonyesha kwamba mahitaji halisi ni chupa 1,250 kwa Mwezi kwa matumizi ya kawaida Unguja na Pemba.Balozi Seif amesema shughuli za uchangiaji wa damu salama  humgusa kila mwana jamii  hivyo ipo faida kubwa inayopatikana licha ya kuokoa maisha ya walio wengi ambao hupatwa na matatizo ya kiafya lakini pia humrahisishia Mtu kuweza kupima maradhi mbali mbali bure bila ya gharama sambamba na kuelewa afya yake.Aliwaasa Wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa maisha yao wenyewe wakiwa kama wana Jamii hasa wanapoelekea katika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani  ambao wengi hushindwa kuchangia Damu kwa wakati  pale wanapokuwa na mgonjwa anayehitaji huduma hiyo kwa haraka.Aliupongeza Uongozi wa Mkoa Kusini Unguja kwa jitihada ulizoonyesha na hatimae kufanikisha zoezi hilo la kuwahamasisha Wananchi wa Makundi mbali mbali kwa ajili ya kuchangia Damu na kukidhi mahitaji ya Maabara  za Hospitali zilizopo Nchini.Akitoa Taarifa ya zoezi hilo Afisa uhamasishaji wa kuchangia Damu kutoka Jumuiya ya Wachangiaji Damu Zanzibar Bwana Bakari Mabarawa alisema hilo ni Bonaza la Tano kati ya Kumi yanayoendelea kufanyika katika Wilaya zote za Unguja na Pemba.Magarawa alisema kufuatia hatua za Wananchi kuhamasika yapo matumaini makubwa ya kuvuka malengo ya matarajio katika Kampeni ya kuhamasisha Jamii kupenda kuchangia Damu salama.Mhamasishaji huyo wa uchangiaji Damu wa Jumuiya ya Wachangiaji Damu alifahamisha kwamba Kituo cha Huduma za Damu Salama bado kimekabiliwa na changamoto ya upungufu wa Watendaji tokea kilipoanzishwa mnamo Mwaka 2008 ambao huathiri zoezi la utoaji Damu pale wanapobahatika kutoa huduma kwenye maeneo yenye idadi kubwa ya Wananchi waliohamasika.Naye Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Hamad Rashid Mohamed  akimkaribisha Mgeni Rasmi kuzungumza na Wananchi hao kwenye Bonaza hilo alisema hilo ni jambo muhimu kwa Uhai na Afya ya Wanaadamu.Mh. Hamad alisema Watu  wote ni wahitajiwa wa kutoa na kupewa Damu Salama jambo ambalo ni wajibu kulisimamia ipasavyo sambamba na kulitekeleza kwa nguvu zao zote.Waziri Hamad aliihakikishia Jamii kwamba Wizara hiyo itajenga mazingira ya uwepo wa Vituo vya Maabara kwa ajili ya kupatikana kwa huduma za Damu salama kwenye Hospitali za Wilaya zote Unguja na Pemba ili kuondosha usumbufu wa kufuata huduma hiyo masafa marefu zilipo Hospitali Kubwa.Bonaza hilo la uchangiaji Damu salama lililoambatana na upimaji wa Maradhi ya Macho, Moyo pamoja na Sukari limeshirikisha Vikosi mbali mbali vya Ulinzi na Usalama, Wananchi wa kawaida pamoja na Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu.