URUSI KUANZISHA UCHUNGUZI JUU YA WITO ALIOUTOA KIONGOZI WA UPINZANI ALEXEI NAVALNY

 

Serikali ya urusi imesema kuwa itaanzisha uchunguzi juu ya wito alioutoa kiongozi wa upinzani alexei navalny wa kutaka wapiga kura kususia uchaguzi wa rais unaotarajiwa mwezi machi mwakani baada ya kuzuiwa na tume ya uchaguzi nchini humo kugombea urais.

Msemaji wa rais vladimir putin, hakuzungumzia kuhusu uamuzi wa tume ya uchaguzi kumzuia navalny kuwania urais, lakini amesema wito wa kutaka uchaguzi kususiwa unachunguzwa kwa makinikwa kuangalia kama kauli ya navalny ilivunja sheria.

Siku ya jumatatu, tume hiyo ya uchaguzi ilimzuia navalny kuwania urais kwa hoja kuwa alihukumiwa kifungo gerezani kwa mashitaka ya uhalifu.

Kiongozi huyo wa upinzani amesema kuzuiwa kuwania urais kunaonyesha ni kwa jinsi gani rais putin anaogopa kushindana naye katika uchaguzi huo.

Umoja wa ulaya umelaani hatua hiyo ya kuzuiwa navalny kugombea urais ikisema ina mashaka iwapo uchaguzi ujao urusi, utakuwa wa haki.