URUSI NA CHINA ZATUMIA KURA YA TURUFU KUISAIDIA SYRIA

 

Urusi na china zimetumia kura ya turufu kuzuia jaribio la umoja wa mataifa la kutaka kuiwekea vikwazo serikali ya syria.

Marekani, uingereza na nchi nyengine katika baraza la usalama, zilitaka kuiadhibu syria kwa tuhuma za kutumia silaha za sumu katika maeneo ya waasi.

Ni mara ya saba sasa urusi inatumia kura yake ya veto kuisaidia serikali ya rais assad na tuhuma za kimataifa.

Balozi wa uingereza katika umoja wa mataifa, matthew rycroft, amesimulia kifo cha mwathirika mmoja ambae alipelekwa katika hospitali baada ya shambulio la gesi yenye sumu nchini syria.

Hata hivyo, kwa upande wake, balozi wa china katika umoja wa mataifa, liu jieyi ameliambia baraza la usalama kwamba bado hakuna vilelezo kwamba serikali ya syria imetumia silaha za kemikali.