URUSI YALIPINGA TENA AZIMIO LA SYRIA

Urusi imepiga tena kura ya turufu kuzuia azimio la umoja wa mataifa linalotaka kuongezwa siku 30 zaidi kwa wataalamu kufanya uchunguzi unaosimamiwa na umoja huo kuhusu mashambulizi ya silaha za kemikali nchini syria.
Hii ni mara ya pili kwa urusi kutumia kura yake ya turufu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kupinga kuanza tena uchunguzi wa pamoja unaojulikana kama jim.
Aidha ni kura ya 11 ya turufu kupinga muswada wa azimio kuhusu syria, mshirika wake wa karibu.
Hatua hiyo itasababisha ugumu zaidi katika kuwabaini waliohusika na shambulizi la kemikali nchini syria.
Kura ya kwanza ya turufu ya urusi kulipinga azimio hilo katika mkutano wa baraza hilo imesababisha kuzorota kwa uhusiano kati ya marekani na ur